• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2017

  SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC juu ya kupokonywa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar mwezi uliopita.
  Simba ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hata hivyo, baada ya mchezo huo, Simba ikakata rufaa Bodi ya Ligi ikidai Kagera Sugar walimchezesha kimakosa beki Mohammed Fakhi kwa sababu alikuwa ametoka kuonyeshwa kadi tatu za njano.
  Simba ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 
  Bodi ya Ligi ikalipeleka suala hilo Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 74 ambayo iliipa ushindi Simba.
  Hata hivyo, Kagera Sugar wakapeleka malalamiko yao TFF wakidai mchezaji wao hakuwa na kadi tatu na Kikao cha Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji kikabatilisha maamuzi ya Kamati ya Saa 72 na matokeo ya Uwanjani yakabaki kama yalivyokuwa.
  Lakini wiki hii, Rais wa Simba, Evans Aveva akasema wanataka kusonga mbele kudai haki yao, lakini wanashindwa kwa sababu hawajapewa barua ya maamzi hayo.
  Na kukata mzizi wa fitina, leo Bodi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Hamad Yahya imeipa barua Simba kuwataarifu kuwa wamepokonywa pointi za mezani.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top