• HABARI MPYA

  Sunday, May 07, 2017

  BUNGE SC YAIFUNDISHA SOKA NMB, YAIPIGA 2-0 NA KUTWAA KOMBE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya benki za NMB.
  Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete ambaye iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.
  Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.
  Spika wa Bunge Job Ndugaia akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu hiyo kuifunga NMB Magori 2-0 wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

  Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali ikiwa na lengo ya kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.
  Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Straton Chilongala akimkabidhi nahodha wa mpira wa Pete wa Bunge Sports Club ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Esther Matiko
  Wachezaji wa Bunge Sports Clun na NMB mpira wa pete wakiwnia mpira wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na wachezaji wa NMB wa Mpira wa kikapu kabla ya mchezo dhidi ya Bunge Sports Club
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BUNGE SC YAIFUNDISHA SOKA NMB, YAIPIGA 2-0 NA KUTWAA KOMBE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top