• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2017

  YANGA NA MC ALGER KIINGILIO BUKU TANO, WAARABU KUWASILI ALHAMISI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga na MC Alger ya Algeria kitakuwa cha Sh. 5,000.
  Mchezo unatarajiwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na viingiklio vingine vitakuwa Sh. 20,000 kwa VIP B na C na 30,000 kwa VIP A.   
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri.
  Mkwasa amesema kwamba wapinzani wao, MCAlger wanatarajiwa kuwasili Alhamisi Saa 3:30 usiku mjini Dar es Salaam, wakati kikosi cha Yanga nacho kitaingia kambini kesho.
  Charles Boniface Mkwasa amesema MC Alger wanatarajiwa kuwasili Alhamisi mchana mjini Dar es Salaam

  Tayari Shirikisho ya Soka Afrika (CAF), limetaja marefa wa Rwanda na Guinea watakaochezesha mechi mbili za mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na MC Alger ya Algeria.
  Mchezo wa kwanza Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utachezeshwa na Louis Hakizimana Atakayepuliza Filimbi Akisaidiwa Na Theogene Ndagijimana na Jean Bosco Niyitegeka wote kutoka Rwanda.
  Mchezo wa marudiano Aprili 14 nchini Algeria utachezeshwa na marefa wa Guinea, ambao ni Yakhouba Keita, Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu.
  Mwaka jana pia Yanga ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambako ilifuzu baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola. 
  Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA MC ALGER KIINGILIO BUKU TANO, WAARABU KUWASILI ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top