• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2017

  SIMBA YAWEKA KAMBI GEITA KUJIANDAA NA MBAO FC

  Na Mwandishi Wetu, GEITA
  SIMBA SC imeweka kambi Geita kujiandaa na michezo yake miwili mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbao FC na Toto Africans.
  Kikosi cha Simba SC kiliwasili jana kwa basi lao kutoka Bukoba, mkoani Kagera ambako Jumapili walifungwa 2-1 na wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
  Na kuelekea mechi dhidi ya Mbao na Toto, Simba SC imeamua kwenda kujificha Geita kwa kambi ya maandalizi ili isirudie makosa ya Jumapili.
  Wachezaji wa Simba kutoka kulia Juuko Murshid, Laudit Mavugo, Abdi Banda na Jonas Mkude

  Na kikiwa mjini hapa, kikosi cha Simba kesho kitamenyana na wenyeji Geita Gold katika mchezo wa kirafiki, sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbao.
  Katika mchezo na Mbao FC, Simba itamkosa Nahodha wake, Jonas Mkude ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWEKA KAMBI GEITA KUJIANDAA NA MBAO FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top