• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2017

  MEXIME AMUANZISHA KASEJA SIMBA NA KAGERA LEO KAITABA

  Na Mahmoud Zubeiry, BUKOBA
  KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amemuanzisha kipa mzoefu, Juma Kaseja kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC ya Dar es Salaam Uwanja wa Kaitaba mjini hapa.
  Mexime amemuweka Kaseja langoni dhidi ya timu aliyopata nayo mafanikio tangu mwaka 2003 hadi 2009 alipohamia Yanga kabla ya kurejea 2011 na kudaka tena hadi 2013 alipohamia Yanga alikocheza kwa misimu miwili kabla ya kuhamia Mbeya Ciy na sasa yuko Bukoba anamalizia soka yake.
  Juma Kaseja (kulia) anaanza leo Kagera Sugar dhidi ya Simba SC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba

  Beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Mtibwa Sugar, Mexime katika safu ya ushambuliaji amewaanzisha pamoja vijana waliobuliwa Simba B, Edward Christopher Shijja na Mbaraka Yusuph Abeid.
  Kwa ujumla, kikosi cha Kagera leo kipo hivi; Juma Kaseja, Godfrey Taita, Mwaita Gereza, Juma Shemvuni, Mohamed Fakhi, George Kavila, Suleiman Mangoma, Ame Ally ‘Zungu’, Edward Christopher, Mbaraka Yusuph na Japhet Makalai.
  Katika benchi Mexime anayesaidiwa na Ally Jangalu atakaa na John Mwenda, Hassan Khatib, Eradius Mfulebe, Antony Matogolo, Ally Ramadhani, Themi Felix, Paul Ngalyoma
  Mchezo huo utachezeshwa Jimmy Fanuel, atakayesaidiwa na Joseph Masija wa Mwanza na 
  Geoffrey Msakila wa Geita, wakati mezani atakuwapo Grace Wamara wa Kagera.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MEXIME AMUANZISHA KASEJA SIMBA NA KAGERA LEO KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top