• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2017

  OMOG AMPANGA MUZAMIL YASSIN KUCHEZA BEKI YA KULIA

  Na Mahmoud Zubeiry, BUKOBA
  KOCHA wa Simba SC, Mcameroon, Joseph Marius Omog amemuanzisha kiungo Muzamil Yassin katika beki ya kulia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Hiyo inafuatia mabeki wote wa pembeni kulia kutokuwa tayari kwa mchezo wa leo, Janvier Besala Bokungu raia wa Jamhuri ya Kixdemokradia ya Kongo (DRC) anamalizia kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Yanga Februari 25 wakati Hamad Juma ni mgonjwa. Bokungu tayari amekosa mechi dhidi ya Mbeya City.
  Muzamil Yassin (kulia) anaanza kama beki wa kulia dhidi ya Kagera leo

  Omog ameweka viungo watatu katikati ambao ni Nahodha Jonas Mkude, Mghana James Kote na Said Ndemla, wakati kulia atachez winga Shiza Kichuya na washambuliaji ni Laudit Mavugo na Ibrahim Hajib.
  Langoni anaendelea kusimama Mghana, Daniel Agyei, kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ katikati Abdi Banda na Juuko Murshid.
  Kwa ujumla kikosi cha Simba leo kipo hivi; Simba SC; Daniel Agyei, Muzamil Yassin, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Laudit Mavuo, Ibrahim Hajib na James Kotei.
  Katika benchi wapo Peter Manyika, Novaty Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Pastory Athanas, Jamal Mnyate, Juma Luizio na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AMPANGA MUZAMIL YASSIN KUCHEZA BEKI YA KULIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top