• HABARI MPYA

  Monday, April 10, 2017

  MAZEMBE YATANGULIZA MGUU MMOJA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo (DRC) jana iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mjini Lubumbashi.
  Mabao yote ya mabingwa hao watetezi wa Kombe la Shirikisho yalifungwa na wageni Uwanja wa Mazembe, la kwanza Mzambia Nathan Sinkala dakika ya 11 na la pili Salif Coulibaly kutioka Mali dakika ya 90.
  Mabingwa mara tatu wa Kombe la Shirikisho, ambayo ni rekodi, CS Sfaxien ya Tunisia walipata ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Rail Kadiogo nchini Burkina Faso.
  Club Africain ilikamilisha ubabe wa timu za Tunisia kwa kuichapa 2-1 AS Port Louis nchini Mauritius, mabao ya Slimene Kchok na Mannoubi Haddad.
  Zesco United ya Zambia walitoka nyuma kwa mabao mawili na kutoa sare ya 2­-2 na Enugu Rangers ya Nigeria huku Patrick Kongolo akisawazisha dakika ya 76.
  Chibuzor Madu alifunga kwa penalti kipindi cha kwanza bao la Rangers na Osas Okoro akafunga la pili kwa "Flying Antelopes" baada tu ya mapumziko.
  Mkenya beki David Owino akafunga bao lake la pili kwenye mashindano ya mwaka huu kwa Zesco, ambayo mwaka jana ilitolewa Nusu Fainali ya Mabingwa.
  SuperSport United ya Afrika Kusini ilitoa sare ya 1-­1 na Barrack Young Controllers nchini Liberia wakati Platinum Stars ilifungwa 2-­0 na AS Tanda nchini Ivory Coast.
  Mapema juzi, KCCA iliwaangusha Al Masry kwa bao 1-0 Uwanja wa Philipo Omondi mjini Kampala, Uganda.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YATANGULIZA MGUU MMOJA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top