• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2017

  LWANDAMINA AMUANZISHA MAKAPU LEO MECHI NA AZAM

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amemuanzisha kiungo Said Juma ‘Makapu’ katika sehemu ya ulinzi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Lwandamina ameshindwa kuendelea kumtumia Kevin Yondan kama kiungo mkabaji kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi na amelazimika kumuamini Makapu, ambaye ataunda safu ya kiungo cha kati cha Yanga kwa pamoja na Mzambia, Justin Zulu.
  Viungo wa pembeni watakuwa Deus Kaseke na Haruna Niyonzima wakati washambuliaji watakuwa Simon Msuva na Mzambia mwingine, Obrey Chirwa.
  Said Juma ‘Makapu’ (katikati) anaanza leo dhidi ya Azam FC jioni ya Uwanja wa Taifa

  Langoni kama kawaida leo Yanga ataanza Deo Munishi ‘Dida’ akilindwa na Juma Abdul kulia, Mwinyi Hajji Mngwali kushoto na Mtogo Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katikati.      
  Lwandamina ambaye leo anamkosa beki wa kulia Hassan Kessy kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi, katika benchi amewaweka; Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Juma Mahadhi, Matheo Anthony, Geoffrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.
  Kocha Mromania wa Azam, Aristica Cioaba naye ameweka viungo watatu katikati ambao ni Himid Mao na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Frank Domayo, wakati kiungo wa pembeni ni Ramadhani Singano ‘Messi’ na washambuliaji ni Yahya Mohmmed na Shaaban Iddi ‘Chilunda’.
  Langoni kama kawaida amemuweka Aishi Manula, beki wa kulia Erasto Nyoni, kushoto Gardiel Michael na katikati ni Waghana Daniel Amoah na Yakubu Mohammed.
  Katika benchi atakaa na akina Mwadini Ali, David Mwantika, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Joseph Mahundi, Masoud Abdallah ‘Cabaye’ na Samuel Afful. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AMUANZISHA MAKAPU LEO MECHI NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top