• HABARI MPYA

  Sunday, April 16, 2017

  KCC YAWATUPA NJE WAARABU WA MISRI NA KUTINGA MAKUNDI

  MABINGWA wa Ligi Kuu ya Azam Uganda, KCCA wameweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza nchini humo kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi.
  Hiyo inafuatia kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-3 mjini Cairo baadaya sare ya kumla ya 1-1 kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani.
  KCCA Jumamosi imefungwa hii imefungwa 1-0 ikitoka kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Phillip Omondi bao pekee la Derrick Nsibambi.
  Kipa Benjamin Ochan leo ameokoa michomo miwili ya penalti na kufunga moja sawa na Geofrey Sserunkuma, Muzamiru Mutyaba na Timothy Dennis Awany kuipa ushindi huo KCCA.
  KCCA iliangukia kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye Ligi ya Mabingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KCC YAWATUPA NJE WAARABU WA MISRI NA KUTINGA MAKUNDI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top