• HABARI MPYA

  Wednesday, August 03, 2016

  MALIMA 'JEMBE ULAYA' APIGA MBILI YANGA IKIWACHAPA BIN SLUM 3-1

  Mshambuliaji wa Yanga Veterani, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' akimtoka beki wa Bin Slum katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Azam Fresco usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-1 na Malima aliyecheza mbele badala ya nafasi yake maarufu, beki alifunga mabao mawili, lingine likifungwa na Nsajigwa Shadrack, wakati bao la Bin Slum lilifungwa na Abuu Ramadhani 'Amokachi'. Yanga sasa inakwenda Nusu Fainali, huku Bin Slum ikiaga mashindano
  Beki wa Yanga, Nsajigwa Shadrack akimuacha chini mchezaji wa Bin Slum

  Kiungo wa Yanga, Ally Yussuf 'Tigana' akiwatoka wachezaji wa Bin Slum

  Deo Lucas akimtoka beki wa Bin Slum

  Mshambuliaji wa Bin Slum, Abuu Ramadhani 'Amokachi' akifumua shuti katikati ya wachezaji wa Yanga 

  Beki wa Yanga, Saleh Hilal akimtoka mchezaji wa Bin Slum

  Shadrack Nsajigwa akienda chini wakati akipambana na Nsa Job

  Kocha wa Bin Slum, Mohammed Bin Slum akiwa haamini macho yake 

  Kikosi cha Bin Slum kilichopigwa 3-1 na jana

  Kikosi cha Yanga jana

  Kocha mwingine wa Bin Slum, Iddi Moshi alitolewa kwa kadi nyekundu kwa kuwatolea lugha chafu marefa jana

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALIMA 'JEMBE ULAYA' APIGA MBILI YANGA IKIWACHAPA BIN SLUM 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top