• HABARI MPYA

  Monday, August 01, 2016

  KUBALI, KATAA LAKINI HAJIB NDIYE MFALME MPYA WA MABAO SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  MSHAMBULIAJI Ibrahim Hajib Migomba ameendelea kumdhihirishia kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog makali yake ya kufunga mabao katika timu ya Simba.
  Hajib wenyewe wanamuita Cadabra wakimfananisha na mshambuliaji mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic leo amefunga mabao mawili, Simba ikiilaza 5-0 Burkina Faso ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.
  Mabao mengine ya Simba leo yamefungwa na viungo Mussa Ndusha kutoka DRC, Shiza Kichuya kutoka Mtibwa Sugar na Said Ndemla.

  Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Simba SC chini ya Omog katika kambi yake ya Chuo cha Biblia mjini hapa kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kuifunga Polisi Moro 6-0 na Moro Kids 2-0.
  Na hayo ni maandalizi ya mchezo dhidi ya Interclube ya Angola Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo maalum wa tamasha la klabu hiyo, maarufu kama Simba Day.
  Interclube wanatarajiwa kuwasili nchini Agosti 6 kabla ya mchezo huo maalum utakaotumika kutambulisha kikosi kipya cha Wekundu wa Msimbazi na benchi la Ufundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUBALI, KATAA LAKINI HAJIB NDIYE MFALME MPYA WA MABAO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top