• HABARI MPYA

  Tuesday, May 03, 2016

  DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MAN UNITED, RASHFORD NAYE ANG'ARA

  WASHINDI WA TUZO ZA MANCHESTER UNITED 

  Mchezaji Bora wa Mwaka: David de Gea
  Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wachezaji: Chris Smalling 
  Mchezaji Bora wa U-21: Cameron Borthwick-Jackson 
  Mchezaji Bora wa U-18: Marcus Rashford
  Bao Bora la Msimu: Anthony Martial v Liverpool   
  Kipa wa Manchester United, David de Gea akipokea tuzo yake Mchezaji Bora wa Mwaka wa timu hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WACHEZAJI wawili wa Manchester United, David de Gea na Chris Smalling wameng'ara katika tuzo za msimu za klabu hiyo inayofundishwa na Louis van Gaal.
  De Gea ameshinda tuzio ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki wa klabu, wakati Smalling ameshinda Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la wachezaji wenzake katika sherehe zilizofanyika usiku wa Jumatatu Old Trafford.
  Kipa wa kimataifa wa Hispania, De Gea amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu akiokoa michomo mingi ya hatari na kuisaidia United kubeba pointi.
  Mshambuliaji kinda, Marcus Rashford ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa umri chini ya miaka 18, wakati beki Cameron Borthwick-Jackson ameshinda Mchezaji Bora kwa vijana chini ya umri wa miaka 21. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MAN UNITED, RASHFORD NAYE ANG'ARA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top