• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2016

  TYSON FURY NA KLITSCHKO KURUDIANA JULAI 9 MANCHESTER

  Tyson Fury (kulia) akizipiga na Wladimir Klitschko (kushoto) katika pambano lao la kwanza Novemba mwaka jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WAPI ULINGO UTAFUNGWA MANCHESTER? 

  Old Trafford (watu 76,000)
  Etihad Stadium (watu, 55,000)
  Manchester Arena (watu 21,000) 
  PAMBANO la marudiano kati ya mabondia wa uzito wa juu, Tyson Fury wa Uingereza na Wladimir Klitschko wa Ukraine litafanyika Julai 9, mwaka huu katika Jiji la Manchester.
  Fury aliustaajabisha ulimwengu alipompiga Klitschko mjini Dusseldorf nchini Ujerumani, Novemba mwaka jana na kutwaa mataji ya dunia ya WBA, WBO na IBF.
  Klitschko akaonyesha dalili za kutaka pambano la marudiano baada ya kipigo hicho cha kushitua, ingawa majadiliano yamechukuwa miezi kadhaa na hatimaye makubaliano yamefikiwa na leo asubuhi pambano limetangazwa.
  Likitarajiwa kufanyika mjini Manchester, Uwanja wa Old Trafford wenye uwezo wa kuchukua watu 76,000 unapewa nafasi kubwa kwa pambano la pili kati ya Fury na Klitschko, dhidi ya Uwanja wa Etihad wenye kukusanya watu 55,000 tu.
  Uwanja mwingine unaoweza kuzungumziwa kwa pambano ni Manchester Arena, ambao ni mdogo zaidi ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 21,000 tu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY NA KLITSCHKO KURUDIANA JULAI 9 MANCHESTER Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top