• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2016

  MAMBO MATANO YA KUJUA KABLA YA 16 BORA LIGI YA MABINGWA

  WAKATI hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika inaanza Jumamosi, BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE inakuletea mambo matano muhimu ya kuzingatia kabla ya mechi za kwanza kesho kutwa.

  1-- Timu tisa zilizowahi kuchukua taji hilo kubwa zaidi Afrika zimeingia hatua ya 16 Bora mwaka huu kuwania kwena hatua ya makundi.

  2-- Miongoni mwao, ni timu tatu zenye mafanikio makubwa zaidi katika michuano hiyo, ambazo ni Al Ahly ya Misri walioshinda mara nane na mahasimu wao, Zamalek waliotwaa mara tano sawa na mabingwa watetezi, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  3-- Mechi kati ya Enyimba ya Nigeria na Etoile Sahel ya Tunisia ni marudio ya fainali ya mwaka 2004 wakati wababe wa Magharibi mwa Afrika walipotwaa taji kwa ushindi wa 2-1 nyumbani.

  4-- Mouloudia Bejaia ya Algeria ndiyo inayocheza kwa mara ya kwanza michuano hii iliyofanikiwa kubaki baada ya kuzitoa AshantiGold ya Ghana katika hatua ya awali ya mchujo na mabingwa wa zamani, Club Africain ya Tunisia katika Raundi ya Kwanza.

  5-- Wydad Casablanca ya Morocco ina rekodi ya kufunga mabao tisa na kufungwa matano baada ya mechi nne dhidi ya Douanes ya Niger na CNaPS ya Madagascar, ikiwafanya kuwa timu iliyofunga na kufungwa mabao mengi.

  RATIBA; Jumamosi Aprili 9, 2016
  Asec MimosasvAhly TripoliRobert ChamprouxSaa 9:30
  Yanga SCvAl AhlyTaifa, Dar es SalaamSaa 10:00
  Stade MalienvZesco UnitedModibo KeitaSaa 1:00
  Wydad Athletic ClubvTP MazembeGrand MarrakechSaa 2:30
  ZamalekvMO BejaiaPetro Sport Saa 3:00
  El MerreikhvES SetifEl Merriekh Saa 3:00
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMBO MATANO YA KUJUA KABLA YA 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top