• HABARI MPYA

    Tuesday, April 19, 2016

    TFF YAZITILIA UBANI AZAM NA YANGA AFRIKA

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao ya Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
    TFF imezitaka Azam FC na Yanga kupambana katika michezo yao ugenini ili kupata matokeo mazuri yatakayozifanya ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, ikiwa kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.
    Azam FC inayoshirki michuano ya Kombe la Shirkisho barani Afrika (CAF CC), leo saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki inashuka dimba la Olymique 07 November, Rades jijini Tunis kuwakabili wenyeji Esperance ST katika mchezo wa marudiano.
    Kesho Jumatano, Yanga SC watakuwa ugenini kuwakabili wenyeji Al Ahly SC katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL), mchezo utakaochezwa saa 12:30 jioni katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZITILIA UBANI AZAM NA YANGA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top