• HABARI MPYA

  Sunday, April 03, 2016

  SAMATTA ATOKEA BENCHI, GENK YAPIGWA 1-0 UGENINI

  MSHAMBULIAJI wa kimatafa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (pichni kushoto) leo ameshindwa kuinusuru na kipigo cha 1-0 ugenini KRC Genk mbele ya RSC Anderlecht katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Pro League.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brussels, Samatta aliingia dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelis, sekunde chache baada ya RSC Anderlecht kupata bao lao.
  Kipa Mholanzi wa Genk, Marco Bizot alijifunga katika harakati za kudaka, bao rahisi zaidi baada ya wenyeji, Anderlecht kupoteza nafasi nyingi za wazi.
  Baada ya Samatta kuingia alijitahidi kutaka kuiokoa timu yake na kipigo hicho, lakini jitihada zake hazikufanikiwa.
  Huo ulikuwa mchezo wa wa saba kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC, akiwa amefunga jumla ya mabao mawili.  
  Kabla ya kufunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya KV Oostende, Samatta pia alifunga katika ushindi wa 3-2 baada ya kuingia dakika 15 za mwisho dhidi ya Club Brugge.
  Mechi nyingine alizocheza Samatta tangu atue Genk, zote akitokea benchi dakika za mwishoni ni dhidi ya Standard Liege (Genk) wakifungwa 2-1, dhidi ya Lokeren wakitoa sare ya 0-0, dhidi ya Waasland-Beveren wakishinda 6-1 na dhidi ya Mouscron-Peruwelz wakishinda 1-0 pia ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI, GENK YAPIGWA 1-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top