• HABARI MPYA

    Tuesday, April 19, 2016

    MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA ESPERANCE

    Winga wa Azam FC, Farid Mussa (kulia) akikimbilia mpira dhidi ya beki Said Mourad 'Mweda' katika mazoezi ya timu hiyo usiku wa leo Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis nchini Tunisia kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.

    Kiungo Frank Domayo (katikati) akifurahia mbele ya kamera ya BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE wakati wa mapumziko mafupi ya kunywa maji 

    Kocha Muingereza Stewart Hall (katikati) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake

    Mshambuliaji Ame Ali (kushoto) akiuvuta mpira mbele ya wachezaji wenzake

    Kiungo Kipre Michael Balou akiambaa na mpira mbele ya mshambuliaji Didier Kavumbangu

    Wachezaji wa Azam FC katika kikao kifupi cha maelekezo kutoka kwa kocha wao Mkuu, Stewart Hall kabla ya kuanza mazoezi  

    Kocha Msaidizi, Mromania Mario Marinica akimpa maelekezo kiungo Himid Mao 

    Mlezi wa Azam FC, Jamal Bakhresa (kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mahmoud Zubeiry (kulia)

    Mangazaji wa Azam TV, Baruwan Muhuza (kulia) akiwa na mpiga picha wake 

    Viongozi mbalimbali wa Azam FC wakifuatilia mazoezi ya timu yao leo uwanjani hapo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA ESPERANCE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top