• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2016

  MALINZI AMPA HEKO GRINDEL KUINGIA OFISINI DFB

  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (pichani kushoto) ametumia salamu za pongezi, Reinhard Grindel kwa kuchaguliwa rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ujerumani (DFB).
  Katika salamu zake kwenda DFB, Malinzi amempongeza Grindel kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ambao hakuwa na mpinzani, na kusema hiyo imeonyesha imani ya watu wa Ujerumani dhidi yake katika maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
  Aidha Malinzi amesema TFF itaendelea kushirikiana na DFB chini ya uongozi wake Grindel katika shughuli za kila siku za maendeleo ya mpira wa miguu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AMPA HEKO GRINDEL KUINGIA OFISINI DFB Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top