• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2016

  KAPOMBE AANZA MATIBABU AFRIKA KUSINI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BEKI  Shomary Kapombe wa Azam FC ameanza kupata matibabu katika hospitali ya Morningside Mediclinic mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Kapombe ameondoka mapema Alhamisi kwenda Afrika Kusini baada ya kuanza kusumbuliwa na Nimonia tangu wiki iliyopita maana yake hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.
  Kapombe aliyekosa mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa sare zote, 1-1 na Toto mjini Mwanza Jumapili na 2-2 na Ndanda Jumatano,hali yake ilizidi kuwa mbaya hadi kusafirishwa Afrika Kusini kwa matibabu.
  Kapombe (kulia) akiwa kwenye ndege wakati wa safari yake Afrika Kusini

  Daktari wa Azam FC, Juma Mwimbe aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba Kapombe hatacheza mechi zote dhidi ya Esperance Jumapili Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.
  Kukosekana kwa Kapombe katika kikosi cha Azam FC wakati huu ambao timu ipo kwenye vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ni pigo.
  Mbali na kuwa mhimili imara wa safu ya ulinzi, Kapombe pia amekuwa mpishi na mfungaji mzuri wa mabao ya timu msimu huu, hadi sasa akiwa amefunga mabao saba kwenye Ligi Kuu pekee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAPOMBE AANZA MATIBABU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top