• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2016

  AMOKACHI: NATAKA KUWAFUNGULIA MILANGO MAKOCHA WA AFRIKA ULAYA

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Daniel Amokachi (pichani kulia) amesema kwamba anataka kuwafungulia milango makocha wa Kiafrika katika klabu za Ulaya.
  Amokachi alitua nchini Finland mwishoni mwa Januari kuanza kazi ya kufundisha timu ya Daraja la Pili, JS Hercules na amesema anataka huo uwe mwanzo wa safari yake ya kufundisha Ulaya. 
  "Ni uzoefu wangu wa kwanza kama kocha wa Afrika kufundisha Ulaya na hakuna Waafrika wengi wanaokochi Ulaya,"amesema nyota huyo wa zamani wa Club Brugge, Everton na Besiktas. 
  "Wamenipa nafasi kama Mwafrika ambayo naweza kuitumia kujipambanua kama nitafanya vizuri, milango iko wazi kwa makocha wengine wa Afrika,”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMOKACHI: NATAKA KUWAFUNGULIA MILANGO MAKOCHA WA AFRIKA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top