• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2016

  WANGA AWATUMIA SALAMU YANGA; "SASA NDIYO MTAMJUA ALLAN WATENDE MAGOLI"

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kuifungia Azam FC bao la ushindi dhidi ya Panone, mshambuliaji Allan Watende Wanga anachofikiria zaidi hivi sasa ni kufunga mabao zaidi kufuatia kuondoa ukame wa mabao uliokuwa umemuathiri kiakili.
  Kauli hiyo ya Wanga imekuja baada ya juzi kuiwezesha Azam FC kushinda mabao 2-1 dhidi ya Panone kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, ukiwa ni mchezo wa raundi ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).
  Wanga alisema alikuwa akilisubiria kwa muda mrefu bao hilo na amelipokea kwa furaha kubwa hasa baada ya kuiwezesha Azam FC kupata ushindi huo.
  Allan Wanga amesema anataka kufunga mabao zaidi Azam FC

  “Nafuraha kufunga kwani sijafanya hivi muda mrefu, nilikuwa na matatizo mengi labda yakaniathiri kiakili, lakini namshukuru Mungu, nashukuru wachezaji wenzangu, nashukuru benchi la ufundi na viongozi wote pamoja na mashabiki kwa sapoti wanayonipa, nimeweza kufunga bao nililokuwa nasubiria kwa muda mrefu.
  “Ujue mshambuliaji ukikaa muda mrefu bila kufunga pia inakuathiri, baada ya kufunga bao hilo la kwanza ni furaha tu niliyonayo, nitaendelea kufanya bidii na kufunga zaidi kwani bao hilo litaniongezea morali zaidi ya kufunga mengine,” alisema.
  Hilo linakuwa bao la pili kwa Wanga ndani ya Azam FC tokea ajiunge na timu hiyo Julai mwaka jana, bao la kwanza alifunga wakati walipoifunga Stand United mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Septemba mwaka jana.
  Wanga anatarajiwa kurudi uwanjani Jumamosi, siku ambayo Azam FC itakuwa inamenyana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WANGA AWATUMIA SALAMU YANGA; "SASA NDIYO MTAMJUA ALLAN WATENDE MAGOLI" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top