• HABARI MPYA

    Monday, March 07, 2016

    TFF YAISHANGAA SIMBA KUMFUNGIA ISIHAKA KIENYEJI, YASEMA ADHABU NI BATILI

    Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema klabu ya Simba haikufuata kanuni katika kumsimamisha Hassan Isihaka.
    Mapema wiki iliyopita uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kumsimamisha beki huyo wa kati Isihaka kwa muda usiojulikana kutokana na kile ulichodai kuwa utovu wa nidhamu ukimtuhumu kutoa ligha chafu dhidi ya kocha mkuu wa muda wa timu hiyo Mganda Jackson Mayanja.
    Hata hivyo, mmoja wa 'vigogo' wa TFF (jina tunalihifadhi) ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE mjini Dar es Salaam jana kwamba mabingwa hao mara 18 wa Tanzania Bara hawakuzingatia matakwa ya Ibara ya 43 ya Kanuni za Ligi za shirikisho hilo toleo la 2015.
    Hassan Isihaka amesimamishwa kwa muda usijulikana Simba SC

    Kifungu cha Pili cha Ibara hiyo, yaani Kanuni ya 43(2), kinasema: "Adhabu zote zitakazotolewa na klabu ni lazima zithibitishwe na TFF kabla adhabu hiyo haijaanza kutekelezwa, TFF inaweza kufuta, kupunguza au kuongeza adhabu ikiwa ni pamoja na kumfungia mchezaji husika nje ya nchi."
    Kiongozi huyo wa juu wa TFF alisema: "Klabu inatakiwa kuwasilisha uamuzi wa adhabu kwa kuwasilisha pia muhtasari wa kikao kilichokaa kuamua adhabu hiyo na vile vile ni lazima mchezaji husika awe amepata nafasi ya kujitetea."
    Kiongozi huyo alizitaka klabu kupitia vizuri kanuni kabla ya kutoa uamuzi wowote kwa kuwa "adhabu za kukurupuka zinaweza kusababisha kuwavuruga wachezaji".
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, aliliambia gazeti hili jana kwamba klabu hiyo ilimuita Isihaka katika kikao hicho na mchezaji alijitetea kulingana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
    Hivi karibuni TFF pia iliwahi kueleza kuwa Yanga ilichemka katika uamuzi wake wa kuvunja mkataba na kiungo wa kimataifa kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima ambaye baadaye ilimrejesha kundini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAISHANGAA SIMBA KUMFUNGIA ISIHAKA KIENYEJI, YASEMA ADHABU NI BATILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top