• HABARI MPYA

  Monday, March 07, 2016

  RATIBA LIGI KUU ‘YABOMOLEWA’ TENA, AZAM FC WAPAA KESHO BONDENI KUWAFUATA BIDVEST

  RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Machi 8, 2016
  Yanga SC Vs African Sports (Saa 10:30 jioni, Taifa, Dar)
  Machi 9, 2016
  Prisons Vs Kagera Sugar (Saa 10:30 jioni, Sokoine, Mbeya)
  Coastal Union Vs Mgambo JKT (Saa 10:30 jioni, Mkwakwani, Tanga)
  Mwadui FC Vs Majimaji (Saa 10:30 jioni, Mwadui, Shinyanga)
  JKT Ruvu Vs Toto Africans (Saa 10:30 jioni, Mabatini, Mlandizi)
  Machi 10, 2016
  Simba SC Vs Ndanda FC (Saa 10:30 jioni, Taifa, Dar)
  Mbeya City Vs Stand United (Saa 10:30 jioni, Sokoine, Mbeya)
  Azam FC wanasafiri Jumatano kwenda Afrika Kusini kuifuata Bidvest Wits

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC iliyokuwa ifanyike Jumatano Saa 10:30 jioni Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro imefutwa na sasa itapangiwa siku nyingine.
  Kufutwa kwa mechi hiyo kumetokana na Azam FC kusafiri keshokutwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya huko.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kwamba mchezo huo sasa utapangiwa siku nyingine baada ya Azam kumaliza majukumu yake ya michuano ya Afrika Raundi ya Kwanza.
  Kikosi cha Azam kinasafiri Jumatano kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza Bidvest Wits unaotarajiwa kufanyika Machi 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Bidvest mjini Johannesburg kuanzia Saa 12.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
  Timu hizo zitarudiana Machi 20, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Esperance ya Tunisia na New Star ya Douala, Cameroon.
  Pamoja na hayo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea kama kawaida katikati ya wiki, kesho mabingwa watetezi, Yanga SC wakiwakaribisha African Sports kuanzia Saa 10:30 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Keshokutwa Prisons itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Coastal Union na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mwadui FC na Majimaji Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, JKT Ruvu na Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani – wakati Alhamisi Simba SC wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mbeya City watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Sokoine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RATIBA LIGI KUU ‘YABOMOLEWA’ TENA, AZAM FC WAPAA KESHO BONDENI KUWAFUATA BIDVEST Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top