• HABARI MPYA

  Saturday, March 05, 2016

  SANCHEZ AINUSURU ARSENAL KUZAMA, MAN CITY YAUA 4-0, CHELSEA SARE 1-1 DARAJANI

  LICHA ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, Arsenal imelazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur katika mechi kali ya Ligi Kuu England  Uwanja wa White Hart Lane.
  
The Gunners walilazimika kucheza sehemu kubwa ya kipindi cha pili wakiwa 10 uwanjani baada ya Francis Coquelin kuonyeshwa kadi nyekundu mwanzoni mwa kipindi hicho.
Spurs wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, walianza mchezo wakiwa pointi tatu mbele ya Arsenal, walitumia mwanya wa kadi nyekundu ya Coquelin dakika ya 55 kufunga mabao mawili ya haraka haraka, kabla ya Alexis Sanchez kufunga bao la kusawazisha kwa Arsenal dakika ya 76.   Nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha timu yake dhidi ya Tottenham leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Arsenal iliyokuwa ikicheza bila kipa wake namba moja, Petr Cech na nafasi yake kuchukuliwa na David Ospina, walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Aaron Ramsey katika dakika ya 36.
Matokeo hayo yameiacha Arsenal nyuma kwa pointi tano dhidi ya vinara wa msimamo, Leicester City.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu ya England leo Manchester City imeifunga 4-0 Aston Villa Uwanja wa Etihad, mabao ya Yaya Toure, Sergio Aguero mawili na Raheem Sterling. Southampton imelazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland Uwanja wa St. Mary's, bao la wenyeji likifungwa na Virgil van Dijk baada ya wageni kutangulia kwa bao la Jermain Defoe.

  Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 wa Manchester City dhidi ya Aston Villa leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  West Ham United imeshinda 3-2 ugenini dhidi ya Everton, mabao ya wenyeji yakifungwa na Romelu Lukaku na Aaron Lennon, wakati ya washindi yamefungwa na Michail Antonio, Diafra Sakho na Dimitri Payet Uwanja wa Goodison Park.
  Chelsea imelazimishwa sare ya 1-1 na Stoke City Uwanja wa Stamford Bridge, bao lake likifungwa na Bertrand Traore kabla ya Mame Biram Diouf kuwasawazishia wageni, wakati Bournemouth imeshinda 3-1 dhidi ya Newcastle United, mabao yake yakifungwa na Steven Taylor la kujifuga,
  Joshua King na Charlie Daniels Uwanja wa St. James' Park, wakati la wenyeji limefungwa na  Ayoze Perez Gutierrez.
  Mchezo mwingine, bao pekee la Gylfi Sigurdsson dakika ya 61 limetosha kuwapa wenyeji, Swansea City ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich City Uwanja wa Liberty.

  Kiungo wa Chelsea, John Mikel Obi akimtoka Giannelli Imbula wa Stoke City leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANCHEZ AINUSURU ARSENAL KUZAMA, MAN CITY YAUA 4-0, CHELSEA SARE 1-1 DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top