• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2012

  KUELEKEA PAMBANO LA WATANI; MARA NYINGI YANGA HUFUNGWA USIKU

  Kutoka kulia; Emmanuel Okwi, Patrick Mafisango (marehemu) na Felix Sunzu wakishangilia bao la penalti alilofunga Sunzu katika mechi ya mwisho ya usiku kukutanisha miamba hiyo. Simba ilishinda 2-0 Agosti 17, mwaka jana Uwanja wa Taifa, je, Jumatano itakuwaje?

  Na Mahmoud Zubeiry
  MECHI ya Jumatano ya watani wa jadi, Simba na Yanga itaanza saa 11:00 jioni na itamalizika kuanzia saa 1:00, wakati giza limekwishaingia uwanjani. Je, unajua matokeo ya mechi zilizopita za watani zilizoishia gizani? BIN ZUBEIRY yupo kwa ajili yako, pata vituz.

  MATOKEO YA MECHI ZA WATANI USIKU:
  JANUARI 1975
  Yanga Vs Simba; Fainali, 2-0
  WAFUNGAJI: Gibson Sembuli na Sunday Manara
  Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati

  JANUARI 1992
  Simba Vs Yanga; Fainali
  1-1, Simba ilishinda kwa penalti 5-4
  Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati

  JANUARI 12, 2011
  Simba Vs Yanga; Fainali 2-0
  WAFUNGAJI: Mussa Mgosi dk 33, Shijja Mkinna dk 71
  (Uwanja wa Amaan, Zanzibar)
  Kombe la Mapinduzi

  OKTOBA 27, 1992
  Simba v Yanga
  1-0
  MFUNGAJI: Damian Morisho Kimti.
  Ligi ya Muungano

  AGOSTI 17, 2011
  Simba vs Yanga 2-0, Dar
  WAFUNGAJI:
  Haruna Moshi ‘Boban’ dk 15 na Felix Sunzu dk 38.
  Ngao ya Jamii
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUELEKEA PAMBANO LA WATANI; MARA NYINGI YANGA HUFUNGWA USIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top