• HABARI MPYA

    Saturday, September 29, 2012

    SIMBA NA YANGA BUKU TANO TU WATU POA

    Emmanuel Okwi wa Simba atakuwa sehemu ya watazamaji Simba na Yanga

    Na Prince Akbar
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetaja viingilio vya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano, Oktoba 3 mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kiingilio cha chini kabisa kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.
    Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja huo kuanzia saa 11:00 kamili jioni na watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
    Wambura alitaja viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
    Kabla ya mechi hiyo itakayorushwa moja kwa moja na Talevisheni ya Super Sport, leo Simba wanaonolewa na Mserbia, Profesa Mserbia Milovan Cirkovick wanacheza na Prisons na kesho Yanga walioleta kocha mpya Mholanzi, Ernie Brandts wanacheza na African Lyon, mechi zote Uwanja wa Taifa.
    Wakati Simba wamefika kambi visiwani Zanzibar, Yanga wapo hapa hapa Jijini, maeneo ya Changanyikeni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA BUKU TANO TU WATU POA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top