• HABARI MPYA

  Saturday, September 29, 2012

  CHEKA AMMALIZA NUSU SAFARI NYILAWILA

  Cheka anatisha

  Na Mahmoud Zubeiry
  FRANCIS Cheka ‘SMG’ wa Morogoro, ameendeleza ubabe dhidi ya mabondia wa Dar es Salaam, baada ya kumtandika kwa Technical Knockout (TKO), raundi ya sita Karama Nyilawila na kutwaa ubingwa wa UBO uzito wa Middle, kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam muda mchache uliopita katika pambano ambalo lilipangwa kuwa la raundi 12.
  Karama aliingia kwa kasi katika pambano hilo na kutumia nguvu nyingi kumshambulia Cheka, ambaye alikuwa mtulivu akipangua na kukwepa ngumi nyingi za mpinzani wake huyo.
  Kuna wakati kwa kasi ya Karama na namna Cheka alivyokuwa akirudi nyuma kwa makonde ya kusukumwa na mpinzani wake, wengi waliamini labda siku ya kuzima ubabe wa bondia wa Morogoro imewadia.
  Hata hivyo, raundi tatu tu zilitosha kumaliza cheche za Karama na tofauti na randi za awali alivyokuwa akirudi kwenye kona yake alikuwa akisimama, lakini baada ya raundi hiyo, aliomba kiti, wakati mpinzani wake aliendelea kusimama.
  Kuanzia raundi ya nne, ilionekana dhahiri Karama ameishiwa nguvu na pumzi na ndipo Cheka alipoanza kumshughulikia.
  Katika raundi ya sita, Cheka aliingia kwa kasi na akafanikiwa kumtandika mpinzani wake upper-cut  na hook iliyomkalisha chini. Alihesabiwa hadi saba, akajikokota kuinuka, lakini mishipa ya kichwa ilikuwa bado haiwasiliani hivyo akaamua kunyoosha mikono yake miwili juu, maana yake; amesalimu amri.
  Hapo ndipo shangwe zilipoibuka katika ukumbi wa PTA, watu wakimpongeza Cheka kuendeleza ubabe wake. 
  Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana

  Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHEKA AMMALIZA NUSU SAFARI NYILAWILA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top