• HABARI MPYA

    Saturday, September 22, 2012

    FALCON YAENDELEA KUGAWA ZANZIBAR


    Na Ally Mohamed, Zanziabr
    MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, Super Falcon wameendelea kuboronga katika ligi hiyo licha ya kumtimua kocha wake wiki iliyopita, baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Jamhuri ya Pemba, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, wakati Bandari imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Uwanja wa Gombani, Falcon ambao wataiwakilisha Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, walikubali kipigo cha tatu mfululizo katika ligi hiyo kwa mabao ya Mfaume Shaaban na Abdallah Mohammed, hiyo ikiwa mechi ya nane kwa Super Falcon kupoteza.
    Bandari iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ilipata bao lake la kwanza dakika ya 37, lililotiwa kimiani na Mussa Omar, kabla ya KMKM kusawazisha dakika ya 44, mfungaji Mudrik Muhib na Bandari wakapata bao la ushindi dakika 76 kupitia kwa Mohammed Abdallah.
    Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi mbili, kisiwani Pemba, Chipukizi wakicheza na Duma Uwanja wa Gombani, huku kisiwani Unguja, Malindi wakicheza na Mafunzo katika uwanja wa Amaan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCON YAENDELEA KUGAWA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top