• HABARI MPYA

    Thursday, September 27, 2012

    BREAKING NEWS: KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA, NI BEKI WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA UHOLANZI ALIYEWEKA REKODI KOMBE LA DUNIA

    Brandts kulia akiwa na Saintfiet wakati wa Kagame

    Na Mahmoud Zubeiry
    BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, ndiye kocha mpya wa Yanga na atawasili wakati wowote kuanzia kesho kusaini mkataba na kuanza kazi.
    Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
    Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
    Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
    Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
    Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
    Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
    Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
    Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
    Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR. 
    Ernie Brandts 1978.jpg
    WASIFU WAKE
    JINA KAMILIErnstus Wilhelmus Johannes Brandts
    KUZALIWA3 February 1956 (age 56)
    ALIPOZALIWANieuw-DijkGelderland
    UREFU1.81 m (5 ft 11 12 in)
    NAFASI ALIYOCHEZABeki (amestaafu)
    KLABU MPYA
    2012 Yanga SC
    TIMU ZA VIJANA
    De Sprinkhanen (Nieuw-Dijk)
    TIMU ZA WAKUBWA
    MwakaTimuMechi(Mabao)
    1974–1977De Graafschap38(2)
    1977–1986PSV Eindhoven251(23)
    1986–1989Roda JC68(4)
    1988–1989MVV Maastricht16(0)
    1989–1991K.F.C. Germinal Beerschot59(5)
    1991–1992De Graafschap20(0)
    TIMU YA TAIFA
    1977–1985Uholanzi28(5)
    TIMU ALIZOFUNDISHA
    1993–2002PSV Eindhoven (timu ya vijana na msaidizi)
    2002–2004RKSV Nuenen
    2005–2006FC Volendam
    2006–2008NAC Breda
    2009Rah Ahan
    2010–APR FC

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWS: KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA, NI BEKI WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA UHOLANZI ALIYEWEKA REKODI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top