• HABARI MPYA

  Friday, September 28, 2012

  AZAM KILELENI LIGI KUU BARA


  Na Prince Akbar
  AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi iliyoanza saa 1:00.
  Mabao ya Azam katika mchezo huo, yalifungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 44 kwa penalti, Kipre Herman Tcheche dakika ya 65 na Kipre Michael Balou dakika ya 79.
  Ushindi huo, moja kwa moja unaipandisha Azam kileleni mwa ligi hiyo, ikifikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kuipiku Simba SC, yenye pointi tisa, lakini iko nyuma kwa mchezo mmopja.
  Kesho Simba itacheza na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, pia mjini Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, wakati Yanga na African Lyon zitapambana keshokutwa kwenye Uwanja huo huo kuanzia saa 11:00 jioni.
  Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1, mwaka huu kuanza saa 10:30 jioni.
  Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikwakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba kuanzia saa 1:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM KILELENI LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top