• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2012

  TATIZO LILIKUWA KIEMBA SIMBA, ILA NYOSSO...

  Jeshi la Jiwe


  Na Mahmoud Zubeiry
  “Amri Kiemba na Jonas Mkude ndio viungo pekee wakabaji katika Simba kwa sasa ambao siku za karibuni hawapangwi- mi nitabaki kuwa mwandishi na mchambuzi, lakini Profesa Milovan Cirkovick ni kocha na mtaalamu, hivyo anajua anachokifanya”.
  Hii ni sehemu ya makala yangu ya BIN ZUBEIRY Septemba 9, mwaka huu, kwa wasomaji wangu wazuri bila shaka watakuwa wanaikumbuka vema.
  Niliandika makala hii, wakati huo Simba inaboronga na katika upangaji wa kikosi, Kocha Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick alikuwa hampi nafasi kiungo Amri Kiemba ‘Jeshi la Jiwe’.
  Baada ya makala hii, naamini ujumbe ulifika na akaanza kumpanga Kiemba, ambaye jana amecheza mechi ya nne tangu Ngao ya Jamii na katika mechi zote timu imecheza vema na kushinda, mchango wake ukionekana ‘wazi wazi’.
  Nilisema katika makala yangu ya Septemba 9, katika soka, kitaalamu mabeki wakiwa wanamrudishia mipira mingi kipa basi kuna tatizo kwenye kiungo pale chini katika kuiunganisha timu na hilo ndilo lilikuwa linajitokeza Simba wakati ule.
  Simba ilikuwa inacheza vizuri ikiwa na mpira, kwa sababu ina viungo wengi wachezeshaji, lakini tatizo linakuja mpira unapohamia kwa wapinzani- wanapita kiulaini na safu ya ulinzi ya klabu hiyo inafikiwa mno, tena kwa urahisi.
  Mipira ilikuwa ikipenyezwa mno kwenye eneo la hatari la Simba- sasa nikasema ni vema kabla ya kuanza kuwatazama mabeki, Simba waimulike safu yao ya kiungo.
  Tazama jinsi Kiemba anavyoiongoza timu kwa sasa, yaani mabeki wanakula raha tu na hata idadi ya mipira ambayo Juma Kaseja amekuwa akirudishiwa imepungua mno, kwa sababu yupo mtu anayeiunganisha timu pale nyuma.
  Kiemba
  Jana Simba imefungwa bao la kwanza katika Ligi Kuu, baada ya mechi tatu na bao lenyewe ni makosa ya watu wawili, Kaseja na Nyosso, kupeana pasi kwenye eneo la hatari bila umakini. Kaseja alimpa pasi Nyosso, kabla hajaumiliki sawa sawa mpira, mtu akaupitia akaenda kufunga.
  Kuna tatizo ambalo Nyosso anatakiwa alifanyie kazi, kuweza kumiliki mpira katika mguu wa pili, fuatilia sana beki huyo kuna mguu ambao hauwezi kabisa kumiliki mpira.
  Ili kujijengea uwezo wa kumiliki mpira kwa miguu yote miwili, Nyosso anatakiwa kufanya mazoezi ya kupiga danadana za miguu yote- kuuchezea sana mpira kwa mguu wa pili. Akiwa mazoezini autumie sana huo mguu unaokataa mpira, ili uuzoee mpira.
  Lakini hata Kaseja anatakiwa kuonyesha maana ya kuzoeana kwake na Nyosso kwa kutompa pasi katika mazingira yale, kwa sababu jana halikuwa bao la kwanza beki huyo anamfungisha kipa wake- si mnakumbuka lile la Davies Mwape?
  Mshambuliaji akimuweka Nyosso kulia kwake, basi atafanikiwa na beki huyo anachoweza kufanya ni kumkwatua tu. Kwa sababu ule mguu mwingine hauwezi kuupitia mpira.  
  Nikirejea kwenye mada, naamini sasa tatizo la Simba limegundulika na limepatiwa tiba, si beki. Ilikuwa kiungo wa chini. Ila sasa, Kiemba ni bindamu na ni mchezaji, kuna kuugua, kuumia au kuwa nje kwa adhabu, nani mbadala wake?
  Yupo dogo Mkude, Milovan anapaswa kumuweka tayari huyu kijana katika programu zake. Nilikuwa nawakumbusha tu, maana kipindi kile wachambuzi uchwara wa kibongo ‘walizomoka’ vitu ambavyo sivyo. Endelea kusoma bongostaz.blogspopt.com ya BIN ZUBEIRY.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TATIZO LILIKUWA KIEMBA SIMBA, ILA NYOSSO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top