• HABARI MPYA

  Tuesday, September 25, 2012

  OKWI HAPONI, KANUNI ZIKIFUATWA HACHEZI SIMBA NA YANGA

  Okwi katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga

  Na Mahmoud Zubeiry
  SIMBA SC, iko hatarini kumkosa mshambuliaji wake hodari wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi katika mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, Emmanuel Okwi iwapo Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, itaamua kufuata kanuni za Ligi zinavyosema.
  Okwi alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja, kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, akilipa kisasi cha kuzewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwa mujibu wa kanuni hilo ni kosa la kufungiwa mechi tatu.
  Hata hivyo, Okwi anaweza kuokoka, iwapo tu ripoti za refa na Kamisaa zitambeba, ingawa hilo ni gumu, kwa sababu hakupewa kadi ya moja kwa moja kwa kucheza rafu wala kuushika mpira kwa makusudi, bali kupiga na hilo adhabu yake ni kukaa jukwaani mechi tatu.
  Tayari Okwi amekosa mechi moja ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, Kamati ya Ligi Kuu inakutana kesho, inatarajiwa kumuongezea mechi mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru kuendelea kumtukia mwajiri wake.
  Siyo siri, kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi ni homa kwa Yanga, hasa wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI HAPONI, KANUNI ZIKIFUATWA HACHEZI SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top