• HABARI MPYA

    Tuesday, September 25, 2012

    MGUNDA AONDOKA NA MANENO 'MAZITO' COASTAL UNION

    Mgunda kulia akiwa na Kondo kushoto 

    Na Mahmoud Zubeiry
    JUMA Mgunda, kocha wa Cosatal Union ya Tanga amesema ameamua kujiuzulu mapema, kabla ya mambo hayajaribika, ili mwalimu mpya anayekuja afanye kazi vizuri.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, Mgunda amesema kwamba anaachia timu baada ya kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akiwa ameshinda moja na kutoa sare mbili.
    “Kama utaweza kuona naiacha timu ikiwa kwenye hali nzuri kuliko Yanga, ambao wamefungwa mechi moja, sare moja na kushinda moja, naondoka kwa moyo mkunjufu, sina kinyongo na mtu,”alisema.
    Mgunda amesema hiyo ndio hulka yake tangu anacheza Coastal Union, kuwa na moyo swafi na ataendelea kuwa hivyo. “Mimi ni mpenzi wa Coastal Union, hakuna asiyejua, na kwa manufaa ya timu, naondoka,”alisema.
    Kumekuwa kama kuna kampeni ya kumvuruga Mgunda kazini ambayo imekuwa ikiendeshwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kumzomea kila timu inapocheza, hatimaye ameamua kuwaachia timu.
    Sasa Coastal, inabaki chini ya kocha Msaidizi, Habib Kondo ambaye msimu uliopita alikuwa kocha wa Villa Squad ya Kinondoni, iliyoshuka daraja.
    Mgunda anakuwa kocha wa pili wa Ligi Kuu kuachia timu, baada ya Mbelgiiji, Tom Sainftiet ambaye amefukuzwa Yanga, baada ya kutofautiana na uongozi, akiwa ameiongoza timu kwenye mechi mbili tu za Ligi Kuu, akitoa sare moja na kufungwa moja.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MGUNDA AONDOKA NA MANENO 'MAZITO' COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top