• HABARI MPYA

    Wednesday, September 26, 2012

    YANGA KUMALIZANA NA PAPIC, NJOROGE KUINUSURU KLABU

    Sanga kushoto, kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Tito Osoro

    Na Mahmoud Zubeiry
    MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema kwamba atayafanyia kazi masuala mawili ya madai dhidi ya klabu hiyo, la aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Mserbia Kostadin Bozidar Papic na beki wao wa zamani, Mkenya John Njoroge, ili kueipushia klabu hiyo hatari ya kuadhibiwa.
    “Mambo haya kwa kweli hatukuwa tukiyajua, ila baada ya taarifa hizi tutayafanyia kazi, ili tuyamalize, tumeingia madarakani tumeyakuta, ila kwa kuwa tumerithi klabu, basi tumerithi yote na hatuna budi kuyafanyia kazi,”alisema Sanga.
    Papic amefungua mashitaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), dhidi ya klabu hiyo, akidai malimbikizo yake ya mishahara, dola za Kimarekani 12,300, zaidi ya Sh. Milioni 15 za Tanzania.  
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja aliiambia BIN ZUBEIRY jana mchana kwamba, wamepokea barua kutoka Kitengo cha Sheria cha FIFA, kikiwataka kuitaarifu Yanga kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na kocha wao huyo zamani.
    Angetile alisema katika malalamiko yake, Papic anadai kuwa hajalipwa malimbikizo ya mshahara wake yanayofikia kiasi cha dola 12,300 za Kimarekani na alikuwa akiwasiliana na maofisa na viongozi waYanga, lakini hakupata ushirikiano na hivyo kuamua kwenda FIFA.
    Angetile alisema TFF ilifanya juhudi za kuwasiliana na Yanga kuhusu malalamiko hayo ili kujaribu kumzuia kocha huyo asishtaki FIFA, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.
    “Na kama chombo kinachosimamia uendeshaji wa soka nchini, TFF imesikitishwa na habari hizo na inaiomba klabu ya Yanga kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa inawasilisha taarifa zote muhimu na nyaraka zinazohusiana na stahiki za kocha huyo ili kama ilishamalizana naye, sifa ya klabu ya Yanga isafishwe,”alisema Angetile.
    Alisema tayari wamekwishaiandikia barua Yanga kuitaka itekeleze utashi huo mapema iwezekanavyo.
    “Tukio hilo, si tu linachafua sifa ya klabu ya Yanga, bali soka ya Tanzania kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba ikishadhihirika kuwa kuna tatizo la malipo ya makocha nchini, ni dhahiri kuwa itakuwa ni vigumu kwa klabu zetu na hata timu za taifa kupata makocha wazuri kutoka nje kwa kuwa watakuwa wamejengeka hofu ya kufanya kazi nchini,”alisema.
    Hili ni tukio la pili kwa Yanga baada ya mchezaji wake mwingine, John Njoroge kuishtaki klabu hiyo FIFA na kushinda kesi yake iliyoamuliwa mwezi Januari na Kitengo cha Usuluhishi wa Migogoro cha FIFA (DRC).
    Alisema ushindi wa Njoroge unamaanisha kuwa iwapo Yanga itashindwa kutekeleza kumlipa mchezaji huyo kasi cha Sh milioni 17, inaweza kujikuta katika adhabu ambayo itailazimisha TFF kuishusha daraja; kuinyang’anya pointi kwa kiwango kitakachotajwa na FIFA; kuipiga faini au adhabu zote kwenda kwa pamoja.
    “Tunaiomba Yanga itekeleze hukumu hiyo kwa wakati uliotajwa kwenye barua ya FIFA ili kuepuka hatua hizo,  suala la Njoroge ni moja kati ya matukio mengi yanayohusu ukiukwaji wa taratibu za kuvunja mikataba yanayofanywa na klabu zetu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUMALIZANA NA PAPIC, NJOROGE KUINUSURU KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top