• HABARI MPYA

  Sunday, September 23, 2012

  SIMBA RAHA NDANI YA RAHA

  Sunzu akimpongeza Edward na Kiemba baada ya kufunga bao la ushindi

  Na Mahmoud Zubeiry
  MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza mabao 2-1 Ruvu Shooting ya Pwani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Shukrani kwake mshambuliaji chipukizi, Christopher Edward aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 80 na kuifanya Simba ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu, nyavu zake zikitikiswa kwa mara ya kwanza leo.
  Simba sasa inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi saba, wakati watani wao wa jadi, Yanga wana pointi nne tu baada ya mechi tatu.   
  Hadi mapumziko, Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya 29, akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’.
  Katika dakika ya 45, kipa Benjamin Haule wa Ruvu Shooting alipangua mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Daniel Akuffor baada ya beki mmoja wa timu hiyo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
  Kipindi cha pili, Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha maarufu nchnini, Charles Boniface Mkwasa ilisawazisha bao dakika ya 80, baada ya Seif Rashid kutumia vizuri makosa ya beki Juma Nyosso dakika ya 75.
  Seif aliupitia mpira miguuni mwa Nyosso, ambaye alianzishiwa na kipa Juma Kaseja na kutokana na kuchelewa kuamua, akasababisha kilichotokea.
  Shukrani wake, chipukizi Edward aliyeifungia bao la ushindi Simba inayofundishwa na Mserbia, Milovan Cirkovick dakika ya 80.
  Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Juma Nyosso, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Edward, Felix Sunzu, Daniel Akuffo/Boban na Mrisho Ngassa.
  Ruvu Shooting; Benjamin Haule, Michael Pius, Mau Bofu, George Michael, Said Suzan, Gideon David, Abdulrahman Mussa, Hassan Dilunga, Paul Ndauka/Seif rashid, Hussein Said na Said Dilunga. 
  Kikosi cha Simba leo

  Manahodha Benjamin Haule wa Ruvu na Juma Kaseja wa Simba wakisalimiana kabla ya mechi

  Hatari kwenye lango la Simba

  Beki MIchael Pius wa Ruvu akiwatoka kiungo Amri Kiemba na beki Amir Maftah wa Simba

  Kiemba akimdhibiti Abdulrahman Mussa, huku Kapombe akiwa tayari kutoa msaada

  Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto akiokoa 

  Kapombe akimdhibiti Hussein Said wa Ruvu

  Kiemba akimkabili Hussein Said

  Kiemba akiondosha mpira miguuni mwa Hussein Said

  Maftah akimdhibiti Said Dilunga

  Benja Haule akipangua penalti ya Akuffo

  Kocha wa Ruvu, Mkwasa akilalamika kwa refa wa akiba, Oden Mbaga kuhusu marefa wa mechi ya leo 
  Mau Boffu akiondosha mpira miguuni kwa Akuffo 


  Chollo akiwatoka Mau Bofu na Abdulrahman Mussa 

  Akuffo anatia krosi

  Mrisho Ngassa anaambaa

  Benja Haule akidaka mpira mbele ya Ngassa, huku akilindwa na mabeki wake 

  Ngassa a napaa

  Benja akidaka mbele ya Sunzu
  Kikosi cha Ruvu Shooting leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA RAHA NDANI YA RAHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top