• HABARI MPYA

  Wednesday, September 26, 2012

  SERENGETI YAJIPIMA TENA NA ASHANTI LEO


  Jacob Michelsen, kocha Serengeti Boys
  Na Prince Akbar
  TIMU ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, leo inacheza mechi ya kirafiki na timu ya Daraja la Kwanza, Ashanti United, ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni, mechi ambayo mashabiki watalipaSh. 500 kuishuhudia.
  Kwa takriban wiki tatu, Serengeti ilikuwa Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Soka Mbeya Mjini (MUFA), ambacho, kiliihudumia kwa malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo na kuweka kambi, ikicheza mechi kadhaa za majaribio ikiwemo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.
  Serengeti Boys ilikuwa icheze na Kenya Septemba 9, mwaka huu mechi ya Raundi ya Kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini wapinzani wao wakajitoa na sasa itacheza na Misri katika Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikichezwa Oktoba 14 mwaka huu, Dar es Salaam na marudiano wiki mbili baadaye mjini Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI YAJIPIMA TENA NA ASHANTI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top