• HABARI MPYA

  Saturday, September 22, 2012

  YANGA YAANZA LIGI, MTIBWA YATOTA CHAMAZI

  Wachezaji wa Yanga, wakimpongeza Kavumbangu baada ya kufunga bao la pili


  Cannavaro anafunga bao la kwanza

  Kiiza na Kavumbangu wakimpongeza Cannavaro
    
  Chuji akimuelekeza Niyonzima namna ya kupiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza 
  DUWA LA KUKU; Wachezaji wa JKT wakiomba dua kabla ya mechi


  Kikosi cha JKT leo

  Kavumbangu akishangilia bao la nne

  Makocha wa Yanga, Freddy Minziro (kulia) na Mfaume Athumani 

  Mwenyekiti wa Yanga, akitoka kwenye chumba cha wachezaji wakati wa mapumziko

  Msuva anafanya safari
  Msuva hatari sana 
  Shamte Ally anamtoka mtu 
  Shamte anashughulika
  Wakubwa wakijipanga kwa kazi
  11 wa Yanga walioanza leo

  Na Mahmoud Zubeiry
  YANGA SC jioni hii imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hadi mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon Msuva.
  Bao la kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada ya Msuva kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao la pili dogo huyo aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja, alimpa pasi mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.
  Kipindi cha pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne dakika ya 65.
  JKT ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.
  Katika mchezo wa leo, Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wakionana kwa pasi nzuri ndefu na fupi, tofauti na ilivyokuwa kwenye iliyopita mjini Morogoro, ambako walifungwa 3-0 na Mtibwa Sugar.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya.
  Yanga leo ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana usiku, kufuatia kutofautiana na uongozi.
  Yanga SC; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
  JKT; Said Mohamed, Kessy Mapande, Stanley Nkomola, Damas Makwaya, Charles Timoth, Ally Khan, Haroun Adolf, Said Ahmed ‘Ortega’/Jimmy Shoji, Omar Changa/Furaha Tembo, Hussein Bunu na Sosstenes Manyasi/Credo Mwaipopo.
  Kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam FC wameifunga Mtibwa Sugar 1-0, bao pekee la Kipre Herman Tchetche, wakati Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha wenyeji JKT Oljoro 1-0 wameifunga Polisi Morogoro, bao pekee la Paul Ndonga dakika ya 13 na  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Coastal Union wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Toto Africans.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA LIGI, MTIBWA YATOTA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top