![]() |
| Coastal Union |
Na Princess Asia
BAO pekee la
Jerry Santo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar leo limeipa ushindi wa 1-0 Coastal
Union katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Zimamoto.
Huo ulikuwa
mchezo wa pili kwa Coastal katika ziara yao ya siku tano visiwani humo,
kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayoanza wiki ijayo. Katika
mchezo wa kwanza, mabingwa hao wa Bara 1988, waliichapa Super Falcon mabao 3-0,
wafungaji Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jerry Santo na Danny Lyanga na Jumapili
Coastal watacheza mechi yao ya mwisho na Mafunzo.
Wimbi hili
la ushindi kwa Cosatal, linafuatia mwendo wa kusuasua kwenye michezo ya
kirafiki ya awali, ilipofungwa mechi nne kati ya tano, kiasi cha kuibuka tetesi
makocha Juma Mgunda na Msaidizi wake, Habib Kondo wanaweza kutupiwa virago.
Ilifungwa na
Azam FC 2-0 Uwanja wa Chamazi, ilifungwa 2-1 na Yanga Uwanja wa Taifa,
ilifungwa 3-2 na Bandari mjini Mombassa, baadaye 2-0 Tanga, ilifungwa 2-1 na
Polisi mjini Morogoro na yenyewe iliifunga JKT Oljoro 1-0 Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.



.png)
0 comments:
Post a Comment