• HABARI MPYA

  Monday, April 01, 2019

  LIVERPOOL YAICHAPA SPURS 2-1 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND

  Mohamed Salah akifurahia na Roberto Firmino baada ya wote kuisaidia timu yao, Liverpool kushinda 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur usiku wa jana Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Firmino alifunga bao la kwanza dakika ya 16 na Salah akasababisha bao la pili ambalo Toby Alderweireld alijifunga dakika ya 90 wakati bao la Spurs lilifungwa Lucas Moura dakika ya 70. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 32 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England sasa ikiizidi Manchester City pointi mbili ingawa imecheza mechi moja zaidi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 61 sasa ikilingana na Manchester United 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA SPURS 2-1 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top