• HABARI MPYA

    Monday, April 15, 2019

    KESSY NA NKANA YAKE WATUPWA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUPIGWA 2-0 TUNISIA

    Na Mwandishi Wetu, SFAX
    SAFARI ya beki Mtanzania, Hassan Kessy na klabu yake, Nkana FC ya Zambia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imefikia tamati kwenye hatua ya Robo Fainali, baada ya kutolewa na CS Sfaxien kufuatia kufungwa 2-0 usiku wa jana Uwanja wa Taieb Mhiri mjini Sfax.
    Matokeo hayo yanamaanisha Nkana inatupwa nje kwa kipigo cha jumla cha mabao 3-2 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Kitwe Aprili 7.
    Katika mchezo wa jana ambao Kessy alicheza kwa dakika zote 90, mabao ya CS Sfaxien yalifungwa na Firas Chaouat dakika ya saba na Alaa Marzouki dakika ya 90.

    Hassan Kessy (kulia) jana klabu yake, Nkana FC ya Zambia imetolewa Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa 2-0 na CS Sfaxien  

    Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho jana, Zamalek iliichapa 1-0 Hassania Agadir ya Morocco Uwanja wa Jeshi la Misri mjini Suez, bao pekee la Ibrahim Hassan dakika ya 49 na kutinga Nusu Fainali kufuatia sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza.  
    Nayo ya RSB Berkane ikaichapa Gor Mahia ya Kenya 5-1 Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco na kutinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 7-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Nairobi. 
    Mchezo kati ya wenyeji, Al-Hilal na Etoile du Sahel ya Tunisa umeahirishwa kwa sababu za machafuko ya kisiasa tangu Desemba mwaka jana nchini Sudan yaliyosababisha Rais Omar Al-Bashir aliyeliongoza taifa hilo kwa zaidi ya miaka 30 kujiuzulu Alhamisi na sasa utapangiwa tarehe mpya. Etoile ilishinda 3-1 Tunisia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KESSY NA NKANA YAKE WATUPWA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUPIGWA 2-0 TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top