• HABARI MPYA

    Wednesday, April 17, 2019

    RAIS WA TFF, KARIA AKATAA KUCHUKUA MGAWO WA 'POSHO' YA CAF DOLA 20,000

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Rais wa TFF kupewa fedha na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zinazodaiwa ni fedha za rushwa.
    Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano,TFF, Cliford Mario Ndimbo imesema kwamba Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Kidao Wilfred amefafanua kwa kina tuhuma hizo.
    Kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF iliyokutana Mei 8,2017 Bahrain kilipitisha maamuzi ya fedha mbalimbali uliokua na mchanganuo wa sehemu ya maendeleo na kiasi kingine kikielekezwa kwa Marais wa Mashirikisho Barani Afrika kuwasaidia katika mizunguko mbalimbali ya mpira wa miguu kwakuwa hawalipwi mshahara.
    Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) akiwa na Katibu wake, Wallace Karia

    Maamuzi yaliyopitishwa ilikua ni kila Shirikisho kupatiwa 100,000 USD ambazo katika mgawanyo huo imeelekezwa Rais wa kila Shirikisho atapatiwa 20,000 USD, Maendeleo Soka la Vijana 50,000 USD na kiasi cha 30,000 USD kusaidia tahadhari kwa Waamuzi.
    Rais wa TFF, Wallace Karia baada ya mgawo huo kuingia aliuelekeza kutumika kwa shughuli mbalimbali za Shirikisho.
    Hivyo basi tunakanusha taarifa zote zinazomuhusisha Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia kuchukua fedha hizo licha ya kuwa zimepitishwa katika vikao halali vya CAF.
    TFF inawasiliana na Wanasheria wake ili wachukue hatua dhidi ya watu wanaosambaza taarifa hizi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS WA TFF, KARIA AKATAA KUCHUKUA MGAWO WA 'POSHO' YA CAF DOLA 20,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top