• HABARI MPYA

    Thursday, April 18, 2019

    CHELSEA NA ARSENAL WASHINDWE WENYEWE EUROPA LEAGUE LEO

    TIMU za Chelsea na Arsenal wanaingia katika michezo ya leo wakiwa na matarajio makubwa ya kufuzu kuingia nusu fainali .
    Arsenal walishinda 2-0 nyumbani kwao dhidi ya Napoli katika mchezo wa kwanza,  huku Chelsea wakishinda ugenini dhidi ya Slavia Prague kwa bao 1-0.
    Hata hivyo Chelsea walifungwa 2-0 ugenini kwa Liverpool na wako hatarini kumaliza msimu nje ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, hii inawaongezea sababu zaidi za kupambana ili kushinda taji la Europa. 
    Mshindi wa Europa hupata tiketi ya moja kwa moja kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya na kwa kusema ukweli hapo ndipo Chelsea na Arsenal wanatamani kucheza.
    Naye mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Chelsea alisema kwamba mchezo wao dhidi ya Slavia Prague ndio mchezo mgumu zaidi ambao wamecheza katika Europa msimu huu. “Watajitahidi kufanya kila kitu ili kufuzu hatua inayofata. Tunajua kiwango chao, kwa hiyo tutajitahidi kumaliza kazi kwenye uwanja wetu”. Alisema
    Mchezo wa Chelsea dhidi ya Slavia Prague utarushwa LIVE kupitia ST Sports Premium pekee, saa 4:00 Usiku.
    Arsenal wanasafiri hadi Italia siku nne tu baada ya kucheza na Watford kwenye ligi na iko wazi kwamba wachezaji wengi hawatacheza kwenye mechi zote mbili kutokana na uchovu na kuepuka majeruhi.
    ‘Gunners’ walilalamikiwa na mshambukiaji wao wa zamani Paul Mariner, ambaye alisema Arsenal walipoteza nafasi nyingi sana kwenye mchezo wa kwanza. “Cha msingi ni ilikuwa ni kumaliza kabisa mchezo. Walikuwa na nafasi  ya kufanya hivyo nyumbani.
    “Sijali wanakwenda wapi, 2-0 kwenye mechi za Ulaya bado mechi haijaisha. Kwa sababu lolote linaweza kutokea, hujui kama mwamuzi atafanya maamuzi sahihi au la, au wachezaji wanaweza wasicheze vizuri,” aliwaambia waandishi. Mchezo wa Napoli dhidi ya Arsenal utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee, saa 4:00 Usiku.
    Kwenye michezo mingine, Valencia walimaliza nusu ya kazi tayari baada ya kushinda ugenini kwa Villarreal 3-1 na sasa wanaweza kufuzu hata wakipoteza mchezo wa nyumbani kwa magoli machache dhidi ya wenzao wa La Liga.
    Mchezo mwingine ni Eintracht Frankfurt dhidi ya Benfica Lisbon, huu bado uko wazi kwa timu zote, japokuwa wareno hao walifunga mabao manne, waliruhusu magoli mawili nyumbani pia.
    Hii inawapa moyo Frankfurt na matumaini ya kufuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1979/80, walipowafunga Borussia Moenchengladbadch kwa bao la ugenini kwenye robo fainali ya wajerumani (kipindi hicho Europa ilijulikana kama UEFA Cup).
    Hakikisha hupitwi na mchezo wowote – angalia kupitia StarTimes pekee, katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa zaidi kwa kulipia Tsh 18,000 tu kwa watumiaji wa Antenna.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA NA ARSENAL WASHINDWE WENYEWE EUROPA LEAGUE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top