• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2019

  RUVU SHOOTING YAITANDIKA MWADUI FC 6-2 MABATINI, MAGANGA APIGA HAT TRICK

  Na Mwandishi Wetu, MLANDIZI
  TIMU ya Ruvu Shooting leo imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 6-2 dhidi ya Mwadui FC.
  Kwa ushindi huo mtamu, Ruvu Shooting inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 29, ikijiinua kutoka nafasi ya 16 hadi ya tisa, wakati Mwadui FC inayobaki na pointi zake 33 baada ya kucheza mechi 29 pia – inateremkia nafasi ya 10.
  Shujaa wa Ruvu Shooting kwenye mchezo wa leo ni mshambuliaji Fully Zulu Maganga aliyefunga mabao matatu dakika za 12, 28 na 69 huku mabao mengine ya Ruvu yakifungwa na Emmanuel Martin dakika ya 13, Tumba Lui Swedi dakika ya 20 na Mussa Said dakika ya 22.

  Mabao ya Mwadui FC jioni ya leo yamefungwa na nyota wake, Salim Aiyee dakika ya tatu na Wallace Kiango dakika ya 60.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leobao pekee la mshambuliaji Ally Ahmed ‘Shiboli’ dakika ya sita limeipa ushindi wa 1-0 JKT Tanzania dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Meja Isamuhyo, wakati KMC leo imelazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
  Na bao pekee la mshambuliaji mkongwe kutoka Burundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika ya 74 limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Alliance FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAITANDIKA MWADUI FC 6-2 MABATINI, MAGANGA APIGA HAT TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top