• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2019

  AUBAMEYANG AKOSA PENALTI SPURS YATOA SARE NA ARSENAL

  Kipa wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris akiokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya mwisho kuinusuru Spurs kuchapwa baada ya kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Wembley leo. Aaron Ramsey alitangulia kuifungia Arsenal dakika ya 16 akimalizia pasi ya  Alexandre Lacazette kabla ya Harry Kane kuisawazishia Spurs kwa penalti dakika ya 74 baada ya kuchezewa na rafu na Shkodran Mustafi. Arsenal ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Lucas Torreira aliyetokea benchi kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Danny Rose. Kwa sare hiyo, Arsenal inafikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 29 ikiangukia nafasi ya tano, wakati Tottenham inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 61 za mechi 29 pia 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG AKOSA PENALTI SPURS YATOA SARE NA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top