• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2019

  LUKAKU APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-2 NA KURUDI 'TOP FOUR'

  Mshambuliaji Mbelgiji, Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya 88 kabla ya Paul Pogba kukosa penalti dakika ya 90 ikiilaza Southampton 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester. Lukaku pia alifunga bao la pili dakika ya 59, kufuatia Andreas Pereira kufunga la kwanza dakika ya 53, wakati mabao Southampton yamefungwa na Yan Valery dakika ya 26 na James Ward-Prowse dakika ya 75 na kwa ushindi huo Man United inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 29 ikipanda nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England nyuma ya Spurs yenye pointi 61 za mechi 29 pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-2 NA KURUDI 'TOP FOUR' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top