• HABARI MPYA

  Monday, August 20, 2018

  WADHAMINI WA SIMBA NA YANGA, SPORTPESA NA EVERTON WASHINDA TUZO ZA SPORTS INDUSTRY

  Na Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
  KAMPUNI ya michezo ya kubashiri SportPesa na Klabu ya mpira wa miguu ya Uingereza ya Everton zimezawadiwa kutoka na ushirikiano wao kwenye tuzo za Sports Industry Awards kwenye vipengele vya Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of the year.
  Kwenye udhamini huo ambao ulianza kwa klabu ya Everton kusafiri kwenda Dar Cup ambao walikuwa ni klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya, umetambuliwa na kusherekewa kwa kuleta klabu inayoshiriki liki kuu ya Uingereza kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza.
  Kutokana na mafanikio ya safari hiyo ambayo ilijulikana kama Everton in Tanzania ambayo ilitoa hamasa kwenye michezo na kuipa ushindi wa tuzo hizo ambazo zilitangazwa Sandton Convention Centre jijini Johannesburg Ijumaa ya tarehe 17 Agosti 2018.
  Katibu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas  wakiwa na tuzo mbili za Sport Industry Awards ambazo kampuni ya SportPesa imeshinda kwenye vipengele vyote viwili.
  Wawakilishi kutoka SportPesa Tanzania, Kenya, South Africa,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania, Timu ya Everton wakipokea tuzo mara baada ya kutangazwa kuwa washindi
  Meneja masoko SportPesa Afrika Kusini, Gail Rodgers, Mkuu wa kitengo cha masoko SportPesa Kelvin Twissa, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas na Mkuu wa kitengo ca Ushirikiano Everton Mark Rollings mara baada ya kukabidhiwa tuzo za Sport Industry Awards.

  Mkuu wa Ushirikiano na Utawala wa klabu ya Everton Mark Rollings alisema ‘ Tunayo furaha kuwa ushirikiano wetu na SportPesa umetambulika kwenye ngazi muhimu ya Sports Industry Awards. Tuzo za Sport Industry Awards ndio tuzo zenye heshima kubwa Africa Kusini kwa upande wa michezo na kwa hivyo kushinda tuzo zote mbili za Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of the Year ni udhibitisho wa kuendeleza ushirikiano wetu na SportPesa pamoja na wadau wake.
  Klabu ya Everton inayo historia nzuri kwa wachezaji kutoka bara la Afrika na muungano maluum na bara hilo, na kwa sababu hiyo sio kwamba leo ni siku ya furaha kwa klabu hii lakini pia inaonyesha ni jinsi klabu ya Everton inayo nguvu ya kuwanyia washirika wake wa kibiashara kwenye ukanda huu. Washirika hawa wawili wamefanya kazi kubwa kwa pamoja kwa miezi kumi na mbili iliyopita kwa kwa uhamashishaji uliofanyika Tanzania msimu uliopita ulikuwa na mafanikio ambapo klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza ilifanya ziara na kucheza na timu kutoka Afrika Mashariki, tukio ambalo lilivuta hisia za watu kutoka ukanda wote huo.
  Mafanikio ya miezi kumi na mbili iliyopita na ishara nzuri ya ushirikiano wetu. Hata hivyo tunaangalia kwa mbeleni jinsi ya kudumisha ushirikiano huu na kuzidi kuwa na nguvu zaidi.
  SportPesa ni kampuni ya kubashiri michezo ambayo anafanya kazi zake Kenya, Tanzania, Afrika Kusini, Italia na UK.
  Mkurugenzi wa Utawalan na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema ‘Ni furaha kubwa kwa SportPesa na mimi binafsi kushuhudia heshima kubwa hii ambayo kampuni imepata kwa kushinda tuzo hizi. Tuzo hizi zitazidi kutupa hamasa ya kuendeleza michezo Barani Afrika na duniani kwa ujumla.
  Akizungumzia kuhusu kuandaa michezo hapa nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Tanzania Susan Mlawi alisema tuzo hizo ni muhimu sana kwa Afrika Mashariki.
  Kuorodhesha na hatimaye kushinda tuzo za Sports Industry Awards kunaonyesha ni jinsi ngani Serikali inatumbua na kuungana mkono michezo nchini Tanzania. Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo inatoa pongezi kwa waandaji wa tuzo hizi kwa kufanya kazi ya uandaaji wa mafanikio. Hii ni ishara njema ya jinsi kumejitolea kuendeleza michezo nchini na kupeleka mpira wa miguu kwenye ngazi ya juu, na kufanya kazi kwa pamoja ili mchezo huo upate mafanikio kwa Tanzania na Afrika nzima. Tumejitolea kufanya kazi kwa upande wetu ili kukuza michezo nchini, alisema Mlawi.
  Klabu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia kwenye michuano ya kwanza ya SportPesa Super Cup kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mbele ya mashabiki zaidi ya 35,000. Mchezo huo ulikuwa na historia kwa Afrika Mashariki kuweza kuwa na timu kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kucheza jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza. Mabingwa wa SportPesa Super Cup, timu ya Gor Mahia kutoka Kenya itasafiri kwenda Uingereza kucheza na klabu ya Everton Novemba 2018 baada ya kutetea ubingwa wake kwa mwaka huu na kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika Mashariki kucheza na timu kutoka Ligi Kuu ya Uingereza mara mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WADHAMINI WA SIMBA NA YANGA, SPORTPESA NA EVERTON WASHINDA TUZO ZA SPORTS INDUSTRY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top