• HABARI MPYA

  Monday, August 20, 2018

  MAMELODI SUNDOWNS YAMCHUKUA MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI WA TANZANIA, HABIB KIYOMBO WA SINGIDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Habib Kiyombo wa Singida United ameondoka mwishoni mwa wiki nchini kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundowns ya huko.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Singida, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba mchezaji huyo atakuwa huko kwa siku 10 akijaribu bahati yake.
  “Sisi kama Singida United sera yetu ni kuona wachezaji wanatoka kwetu na kwenda mbali zaidi, ndiyo maana tumemruhusu Kiyombo na tutafurahi akifanikiwa Mamelodi Sundowns,”amesema Festo.

  Habib Kiyombo amekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio Mamelodi Sundowns 

  Sanga amesema Kiyombo ambaye alijiunga nao Juni akitokea Mbao FC ya Mwanza hajaacha pengo Singida United, kwani timu ina kikosi kipana chenye wachezaji 30, hivyo kutokuwepo kwake kwa siku 10 si tatizo.
  “Na tunamuombea kabisa afanikiwe achukuliwe na hiyo timu kwa sababu hiyo ndiyo sera yetu na tutafurahi akichukuliwa na timu kubwa kama hiyo,”amesema.
  Katika hatua nyingine, Festo amesema kwamba kocha Mkuu, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amejiunga na timu kwa maandalizi ya mwisho kufuatia kugoma awali kutokana na tofauti zake na uongozi.
  “Morocco amekwishajiunga na timu, wiki ya pili sasa na tunaendelea na maandalizi ya mwisho mwisho ya Ligi Kuu,”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI SUNDOWNS YAMCHUKUA MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI WA TANZANIA, HABIB KIYOMBO WA SINGIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top