• HABARI MPYA

  Monday, August 20, 2018

  AZAM FC KUWAKOSA KIPAGWILE NA LYANGA MECHI NA MBEYA CITY ALHAMISI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wawili wa Azam FC walioumia kwenye kambi ya Uganda, winga Idd Kipagwile na mshambuliaji Danny Lyanga wameanza mazoezi mepesi – maana yake hawataweza kuhusika katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City. 
  Azam watakuwa wenyeji wa Mbeya City Alhamisi kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kipagwile na Lyanga hawako tayari kwa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
  Pamoja na hao, Azam, FC itawakosa majeruhi wengine Joseph Kimwaga na mshambuliaji Donald Ngoma ambao wanaendelea na programu maalum ya mazoezi ili kujiweka fiti.

  Azam FC itamkosa Daniel Kyanga katika mechi za mwazno za Ligi Kuu

  Azam FC iliyokuwa Uganda kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya, jana ilianza kujifua zikiwa baada ya kurejea nchini zikiwa zimesalia siku tano tu kuelekea mchezo na Mbeya City ambao unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Kocha Msaidizi wa Azam FC, Juma Mwambusi, ameshaweka wazi kuwa kambi ya Uganda imewasaidia kuwaweka pamoja na wachezaji na kilichobakia hivi sasa ni kurekesbisha mapungufu kadhaa kabla ya kuingia kwenye ligi wiki ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUWAKOSA KIPAGWILE NA LYANGA MECHI NA MBEYA CITY ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top