• HABARI MPYA

    Tuesday, August 21, 2018

    MAREFA 82 WAPITISHWA KUCHEZESHA LIGI KUU MSIMU WA 2018-2019

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepitisha marefa 82 kuchezesha Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2018/2019.
    Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati 30,Waamuzi wasaidizi 46 na Waamuzi 6 wa akiba.
    Waamuzi hao ndio watakaokuwa na jukumu la kucheza mechi zote za Ligi Kuu katika msimu husika.
    Na uteuzi huo umefanyika baada ya mtihani wa vipimo kwa waamuzi hao uliofanyika mjini Dar es Salaam mapema mwezi huu.
    Waamuzi waliopitishwa na ni Athuman Selukala (Arusha), Erick Onoka (Arusha), Alex Magayi (Dar es Salaam), Elly Sasii (Dar es Salaam), Isihaka Mwalile (Dar es Salaam), Israel Nkongo (Dar es Salaam), Mbaraka Rashid (Dar es Salaam), Nadim Aloyce Leonard (Dar es Salaam) na Liston Hiyari (Dar es Salaam).

    Wengine ni Florentina Zabron (Dodoma), Ally Simba (Geita), Amada Simba (Kagera),Jonesia  Rukyaa (Kagera), Hussein Athumani (Katavi), Shomari Lawi (Kigoma), Alfred Vitares (Kilimanjaro), Jacob Adongo (Mara) na Benedict Magai (Mbeya).
    Wengine ni Athumani Lazi, (Morogoro), Fikiri Yussuf (Morogoro), Martin Saanya (Morogoro), Abubakar Mturo (Mtwara), Daniel Warioba (Mwanza), Emmanuel Mwandembwa (Mwanza), Ludovick Charles (Mwanza), Ahmad Seif Mbaraka (Pwani), Nassoro Mwinchui (Pwani), Jimmy Fanuel (Shinyanga), Meshack Suda (Singida) na Hance  Mabena wa Tanga.
    Waamuzi wasaidizi au washika vibendera waliopitishwa ni Agnes Pantaleo (Arusha), Abdallah Uhako (Arusha), Gasper Keto (Arusha), Frank Komba (Dar es Salaam), Germina Simon (Dar es Salaam), Hamisi Chang'walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Iddi Mikongoti (Dar es Salaam) na Kassim Mpanga
    (Dar es Salaam).
    Wengine ni Lulu Mushi (Dar es Salaam), Omary Kambangwa (Dar es Salaam), Shaffi Mohamed (Dar es Salaam), Soud Lilla
    (Dar es Salaam), Charles Simon (Dodoma), Godfrey Msakila (Geita), Janet Balama (Iringa), Rashid Zongo (Iringa)Edgar Lyombo (Kagera) na Grace Wamala (Kagera).
    Wamo pia Jamada Ahmada (Kagera), Athumani Rajab (Kigoma), Soud Hussein (Kigoma), Sylvester Mwanga (Kilimanjaro), Leonard Mkumbo (Manyara), Robert Ruemeja
    (Mara), John Kanyenye (Mbeya), Mashaka Mandembwa (Mbeya), Jesse Erasmo (Morogoro), Nickolas Makaranga
    (Morogoro), Consolata Lazaro (Mwanza), Frednand Chacha
    (Mwanza), Josephat Masija (Mwanza), Michael Mkongwa (Njombe), Abdallah Rashid (Pwani) na Kassim Safisha (Pwani).
    Wengine ni Khalfani Sika (Pwani), Japhet Kasiliwa (Rukwa), Joseph Pombe (Shinyanga), Julius Kasitu (Shinyanga), Makame Mdogo (Shinyanga), Arnold Bugardo
    (Singida), Justina Charles (Tabora), Martin Mwaliaje (Tabora), Nestory Livangala (Tabora), Haji Mwarukuta (Tanga) na Mohamed Mkono (Tanga).
    Waamuzi wa akiba waliopitishwa ni Steven Daudi Makuka (Iringa), Ahmadi Benard Augustino (Mara), Ally Mkonge (Mtwara), Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Shaaban Msangi (Singida) na Omary Mdoe (Tanga).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA 82 WAPITISHWA KUCHEZESHA LIGI KUU MSIMU WA 2018-2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top