• HABARI MPYA

    Wednesday, August 29, 2018

    KUTINYU: USHIRIKIANO NDIYO SIRI YA MAFANIKIO NDANI YA AZAM

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mshambuliaji wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati na Kati Azam FC, Tafadzwa Kutinyu, ameweka wazi mabao mawili aliyofunga Jumatatu yalitokana na ushirikiano ndani ya kikosi hicho.
    Kutinyu alifunga mabao hayo wakati Azam FC ikiilaza Ndanda mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam, bao lingine la likifungwa na Joseph Mahundi.
    Mzimbabwe huyo aliyesajiliwa msimu huu akitokea Singida United amesema siri ya mafanikio yao uwanjani ni kucheza kama timu na kila mchezaji kumsisitiza na kumsapoti mwenzake.

    Tafadzwa Kutinyu amesema ushirikiano ndiyo siri ya mafanikio ndani ya kikosi cha Azam FC

    “Tunacheza pamoja kwa ushirikiano kama timu na kila mmoja kumpa sapoti mwenzake, nimefurahi sana kufunga mabao mawili jana na namshukuru Mungu kwa kuniwezesha hilo,” alisema.
    Akizungumzia kucheza mechi yake ya pili msimu huu, alisema kuwa: “Nina furaha kwa sababu tunafanya kazi pamoja kama timu na mimi namuheshimu kila mmoja kwa sababu Azam inao wachezaji bora hivyo tunasaidia kwa pamoja, tunasali na kuendelea kupambana na Mungu atafanya kwa mujibu wa mapenzi yake.”  
    Aidha alisema kuelekea mechi zao zijazo wataendelea kupambana kuhakikisha wanavuna pointi nyingine tatu ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.
    Kutinyu na Mahundi kwa pamoja wote wamefunga mabao mawili kila mmoja kwenye mechi mbili za ligi walizocheza hadi sasa, huku mshambuliaji Danny Lyanga, akifunga bao jingine lililobakia ambalo ni la tano kwa msimu huu.
    Azam FC waliotwaa ubingwa wa Kombe la Kagame mara mbili mfululizo pamoja na lile la Mapinduzi, imefikisha jumla ya pointi sita na kurejea kileleni kwenye msimamo wa ligi ikizizidi mabao ya kufunga Simba na Mbao ambazo nazo zimejikusanyia idaidi hiyo ya pointi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUTINYU: USHIRIKIANO NDIYO SIRI YA MAFANIKIO NDANI YA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top